China inamtuhumu Pompeo kwa kusema uongo

China imemtuhumu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo kwa kile ilichosema kuzungumza uongo kwa lengo la kufutikiza muendelezo wake wa ulaghai dhidi ya serikali ya Beijing, kuhusu janga la corona.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China, Hua Chunying, alisistiza kwa serikali ya China imekuwa na uwazi kuhusu mripuko wa ugonjwa wa COVID-19 ambao ulianzia katika ardhi ya taifa hilo mwishoni mwa mwaka uliopita.

Na kwamba wanasiasa wa Marekani wanatoa tuhuma zisizo na msingi wowote. Marekani inaituhumu China kwa kushindwa kuudhibiti mripuko.

Vile vile Hua alisema serikali ya China inapinga kitendo cha Marekani kuingilia masuala yake ya ndani, akijubu uamuzi wa Wizara ya Mambo ya Nje kuchelewesha ripoti kwa bunge la Marekani inafuatilia kama Hong Kong inafurahia mamlaka yake kutoka China, ili iweze eneo hilo liweze kuchukuliwa kwa namna ya kipekee na Marekani.

Mpya zaidi Nzee zaidi