Kituo cha runinga cha CNN chapongeza Uturuki ilivyokabiliana na Covid-19

Kituo cha ruinga cha Marekani CNN chapongeza Uturuki ilivyokabiliana na virusi vya corona.

Kituo cha ruinga cha Marekani , kitengo cha kimataifa kimepongeza Uturuki  namna ilivyokabiliana na mbinu ilizotumia kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona.

Kituo hicho kimetaarisha na kupeperusha makala  ambayo inazungumzia Uturuki  ilivyokabiliana kwa mafaanikio  dhidi ya virusi vya corona.

Kituo hicho kimefahamisha kuwa Uturuki imefualu vita vyake dhidi ya covid-19.

Waziri wa Afya wa Uturuki Fahrettin Koca amepeperusha kupitia ukurasa wake wa Twitter  kuhusu makala hiyo iliozungumzia Uturuki ilivyokabiliana na virusi vya corona.

Makala hiyo ilirushwa Mei 3 kupitia runinga hiyo ya CNN  kitengo cha kimataifa.

Katika makala hiyo, mbinu zilizotumiwa na  Uturuki katika kupambana na maambukizi ya  covid-19  zimezungumziwa na kuonekana mbinu zilizostahili katika zoezi hilo  dhidi ya virusi.
Mpya zaidi Nzee zaidi