China imezindua chombo cha anga za juu kilichopewa jina la Tianwen-1 kuelekea katika sayari ya Meriki au Mars kwa Kiingereza, ikiwa ni ziara ya kwanza na yenye changamoto nyingi, katika juhudi za nchi hiyo kupigania hadhi ya kuwa miongoni mwa mataifa yanayofanya utafiti katika anga za juu na kuingia katika kundi sawa na Marekani na Urusi.
Tianwen-1, ambayo maana yake ni Maswali juu ya Mbingu, ni chombo kinacholenga kufanya utafiti katika mazingira ya sayari ya Meriki na kutafuta uwezekano wa dalili za maisha katika sayari hiyo.
Chombo hicho kitasafiri kwa takriban miezi saba kabla ya kuifikia sayari hiyo, na kitaizunguka kwa miezi miwili au mitatu kabla ya kujaribu kutua.