UN yatoa wito wa mapato ya msingi kuwasaidia watu maskini zaidi katika vita dhidi ya corona

Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP limesema kuwa takriban watu bilioni tatu maskini zaidi duniani wanapaswa kupewa mapato ya msingi kwa muda kusaidia kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona.

Ripoti ya shirika hilo iliyochapishwa jana, imesema kuwa huku idadi ya maambukizi ikiongezeka katika mataifa yanayoendelea, mikakati ya kuwalinda watu walio katika mazingira magumu inahitajika kwa haraka.

Ripoti hiyo imesema fuko la dola bilioni 199 kwa mwezi linaweza kuwapa watu bilioni 2.7 mapato ya msingi ya muda na njia ya kununua chakula na kulipia gharama za matibabu na elimu.

Makadirio ya Umoja wa Mataifa yameonya kuwa virusi vya corona huenda vikasababisha vifo vya watu milioni 1.67 katika mataifa 30 yalio na mapato ya chini.

Mpya zaidi Nzee zaidi