Na Ahmad Mmow, Nachingwea.
Wakati vyama vya siasa vikiandaa wanachama wake watakaogombea nafasi za urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Zanzibar, wabunge, wajumbe wa baraza la wawakilishi na madiwani katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu wa 2020.
Kiongozi mkuu wa chama cha Alliance for Change and Transparency ( ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe ametoa wito kwa vyama makini na vyenye nguvu vishirikiane.
Zitto ametoa wito huo leo mjini Nachingwea alipokuwa anazungumza na wanachama wa chama hicho na wengine wenye mapenzi na chama hicho kupitia mkutano wa ndani.
Zitto alisema kunahaja ya vyama makini vya upinzani nchini vishirikiane katika uchaguzi huu ili viwe na nguvu zitakazotumika kupambana kukiondoa CCM.
Katika hali iliyoonesha kwamba alichokuwa anasema ndicho anachokiamini nakukiishi, alisema tofauti ndogondogo baina ya vyama hivyo zisiwe kikwazo cha kushirikiana. Bali vikae chini nakutafakari ni mgombea wa chama gani na waeneo gani anakubalika kwa wapiga kura ili aachiwe eneo hilo.
Zitto alionya kuwa vyama makini havina sababu ya kutengana. Kwani madhara yake nimakubwa kuliko faida, hasa kwa wananchi.
Aidha kiongozi mkuu huyo wa ACT-Wazalendo alivitahadharisha vyama vya upinzani viache tabia ya kubomoana na kudhoofishana. Hasa vyama vyenye nia ya kweli ya kutaka mabadiliko.
Katika kuonesha anasimamia hilo kwavitendo aliwataka wanachama wa vyama vingine vya upinzani waliokuwepo ndani ya ukumbi huo wabaki kwenye vyama vyao wasijiunge na chama hicho.
'' Mkiona huko juu hatuelewani, nyinyi shirikianeni. Mkiona mgombea wa chama fulani ananguvu eneo fulani muungeni mkono. Mtazame nguvu za wagombea bila kujali anatoka chama gani! muhimu ni kushinda,'' Zitto alisisitiza.
Zitto bila yakuingia kwa undani zaidi kueleza sababu za kushinda na kukiondoa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni kwamba serikali inathamini maendeleo ya vitu kuliko watu. Nakwamba inashughulika na vitu badala ya watu.
