Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa asema kuna uwezekano wa kufanya mazungumzo na magaidi Afrika


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema jana kuna uwezekano wa kufanya mazungumzo na makundi kadhaa ya kigaidi yanayofanya mashambulizi yake katika eneo la Sahel. 

Guterres lakini anasema hawawezi kufanya mazungumzo na makundi yenye misimamo mikali mno kama lile linalojiita Dola la Kiislamu.

 Sehemu kubwa ya eneo la Sahel lina ukosefu wa usalama na mashambulizi ya kigaidi yalianza baada ya kuzuka uasi kaskazini mwa Mali 2012. 

Machafuko hayo yameenea hadi katikati mwa nchi hiyo na hata katika nchi jirani za Burkina Faso na Niger na kusababisha vifo vya maelfu ya watu. 

Matamshi haya ya Guterres yamekuja wiki moja baada ya Kamishena wa Amani na Usalama katika Umoja wa Afrika Smail Chergui kutaka mazungumzo yafanyike na makundi ya kigaidi.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi