CHADEMA yalaani vitendo vya kikatili kwa wanawake na watoto


CHADEMA walia na ukatili wa kijinsia walaani vitendo hivyo kuendelea k,uwepo kipindi hiki cha Sayansi na Tekenolijia.

Akiongea kwenye mkutanp wa kampeni jana uliokalia viwanja vya Songambele (B)katibu mwenezi wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA),Pamba Chacha Mwita ambaye pia ni mgombea kata ya Sabasaba ambae aliwekewa pingamizi na barua ya kugombea hawajapewa na mkurugenzi wa halmashauri ya mji,Elias Ntiruhungwa alisema kuwa kuna haja maadhimisho hayo kufanyika Tarime kutokana na  vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto kukidhiri.

“Mh mgombea ubunge wa Chadema jimbo la Tarime mjini,Esther Matiko kwa kuwa umefanyiwa ukatili mwingi kipindi hiki cha uchaguzi ikiwemo mmoja wa Askari polisi kukutendea ndivyosivyo huku akikudhalilisha bila kujali miiko ya Ajira kuna haja maadhimosho ya  wanawake Duniani ya kupinga ukatili yanayofanyika kila mwaka Mchi,08 kufanyika Tarime ili wanawake kupaza sauti ya kupinga vitendo hivyo”alisema Pamba.

Pamba aliongeza kusema kuwa Chama chake kimejipanga kushinda licha ya mgombea wake kutendewa ukatili huku akidhalilishwa kwa sababu ni mwanamke wataenda kushinda kwa nguvu ya umma na watatangazwa.

Naye Bashiri Selemani (SAUTI) alitumia nafasi hiyo kuwataka wapiga kura kukiamini chama cha Chadema na kuwapa kura ili kuingia Ikulu na kuwaletea maendeleo huku wakirekebisha baadhi ya sheria.

Sauti alisema kuwa akipewa ridhaa ya kuwa Diwani ndani ya kata ya Nysamisangura ataenda kuboresha Afya kwa wanakata wake pale ambapo atajenga kituo cha Afya pia Sauti alitumia kipengere cha 8 cha katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania kujinadi ili wananchi kumpa kura  endapo mkurugenzi wa uchaguzi,Elias Ntiruhungwa atawapa barua ya kugombea baada ya kiuwekewa pingamizi na kukata rufaa Tume ya Taifa ya uchaguzi.

Kwa upande wake mgombea ubunge jimbo la Tarime,Esther Matiko alisema kuwa kuna poropoganda kutoka kwa wapinzani wake wa Chama cha mapinduzi kuwa alipokuwa mbunge hajafanya maendeleo ambapo alisema kuwa amejenga darasa katika shule ya msingi Sabasaba kwa kutumia fedha yake ya mfukoni.

Matiko aliongeza kuwa endapo wananchi watampa kura tena mwakwa huu  kwa mara nyingine ataenda kufanyia wazo lake la kujenga Gorofa ndani ya shule hiyo ili kuondoa usumbufu wa wanafunzi kusoma kwa zamu  ambapo alisema kuwa wazo hilo awali  lilikwama kutokana na kutopewa BOQ na kutekelezeka akamalivyoahidi.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi