Na Omary Mngindo, Ruvu
KIKUNDI cha watu 30 wenye ulemavu wa viungo mbalimbali katika Vijiji vinavyounda Kata ya Ruvu Jimbo la Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani, wanahitaji shilingi milioni 15 kwa ajili ya mtaji wa biashara.
Kikundi hicho kinachohusisha walengwa hao kimetokana na ulemavu uliosababishwa na matukioa mbalimbali, wakiwemo walioshambuliwa na mamba walipokwenda mtoni aidha kuvua samaki au kuchota maji ndipo wakakutwa na mikasa hiyo.
Wakizungumza kwa niaba ya wenzao, muda mfupi baada ya mkutano wa Kampeni wa mgombea Ubunge Jimbo hilo Michael Mwakamo, Selemani Mlowe Katibu na Idd Maro walisema kuwa halo waliyokuwa nayo imeluwa changamoto kubwa kwao.
Mlowe lisema kuwa kikundi hicho kilichoweza kukopa shilingi milioni mbili kupitia Halmashauri ya Kibaha, pamoja na kujitahidi kurejesha lakini wamekwama kutokana na shughuli zao za kilimo kukumbana na changamoto ya mifugo.
"Kutokana na kuwepo kwa changamoto ya mifugo tumeona bora tutafute wahisani wataptupatia mtaji wa boashara wa shilingi milioni 15, ili tuachane na kilimo kwani mifugo haitoweza kuingia ndani, hivyo hatua hiyo itakuwa msaada mkubwa kwetu," alisema Mlowe.
Nae Maro alisema kuwa kikundi chao chenye wanachama hao 30 kilikopa milioni 2 kutoka Halmashauri lakini mpaka leo wanasuasua kuulipa, hivyo kuwaweka katika mazingira magumu kiuchumi, huku akirlrkeza masikitiko yake kuhusiana na mifugo.
"Mpaka sasa tumejitahidi kurejesha mkopo lakini bado hawajamalizo kutokana na kilimo wanachokitegemea kukumbwa naa changamo ya mifugo, ambapo kabla ya kuvuna mifugo inaingia hivyo kula mazao," alisema Maro.
Aidha mkazi huyo alielezea sababu za ulemavu wake wa mguu uliotokana na kuchomwa na mwiba, ambapo alilazwa Tumbi miezi sita, tatizo lililosababisha mguu wake kuwa mfupi.
Aidha wakazi hao wamemuombea dua mgombea Ubunge jimboni humo Michael Mwakamo ili achaguliwe kushika nafasi hiyo, huku wakimtaka alikumbuke kundi hilo katika kuwatafutia wahisani wataowasaidi katika nyanja mbalimbali.
