Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) limeripoti kuwa litahifadhi sindano milioni 520 kwa ajili ya chanjo dhidi ya corona.
Katika taarifa iliyotolewa na UNICEF,Imeelezwa kuwa chanjo ya corona imeanza kufanyiwa maandalizi muhimu ya kusambazwa haraka, salama na kwa ufanisi.
Katika taarifa hiyo, ambayo imesema kuwa sindano zitahitajika kwa mamilioni ya chanjo baada ya chanjo ya Covid-19 kukamilika na kuwa tayari kwa matumizi, imebainika kuwa UNICEF itafanya akiba ya sindano milioni 520 na mapipa milioni 5 ya taka ya kuondoa sindano zilizotumika kufikia 2021.
