Nisha atamani kuolewa na Ommy Dimpoz

 


Staa wa filamu nchini Nisha Bebe ambaye kwasasa amejikita kwenye biashara ya mavazi, ameeleza kukoshwa na picha mpya za msanii Ommy Dimpoz akiwa Makka hadi kupelekea kutamani kuolewa na mkali huyo.

Ommy Dimpoz ambaye kwasasa yupo nchini Saudi Arabia kwa ajili ya kufanya Ibada ya Umrah, Nisha Bebee amesema Dimpoz amefanya kitu kikubwa sana na amemshawishi na yeye kwenda kufanya tukio hilo la kuhiji kama ilivyokuwa kwa marehemu Mzee Majuto.

"Yaani sijawahi kuona picha ya mtu nikatamani kuolewa naye, mara baada tu ya kuiona hii picha nimetamani kuolewa na Ommy Dimpoz na ni kitu ambacho hata akilini mwangu hakikuwepo, umefanya kitu kikubwa sana"

"Serious wa kwanza kunishawishi kutamani kuhiji ni marehemu baba yangu Mzee Majuto, Ommy umenikumbusha vitu vingi sana, kiukweli nimejiskia raha kutoka moyoni kwa hiki ulichofanya" ameeleza Nisha Bebee kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Nisha Bebe amsisitizia Ommy Dimpoz asirudie makosa aliyowahi kuyafanya na aendelee kuishi kwenye mstari ulionyooka mpaka mwisho wa maisha yake.


Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi