Mchezo wa ligi kuu Tanzania VPL Na. 259 (Simba SC vs Coastal Union FC) uliopangwa kuchezwa Mei 11, 2021 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijininDar es Salaam, umeahirishwa na sasa utapangiwa tarehe nyingine.
Taarifa iliyotolewa na TFF imeeleza kuwa sababu ya mabadiliko hayo ni kutokana na changamoto za usafiri kwani Simba italazimika kusafiri siku hiyo (Mei 11) kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya mchezo wa CAFCL dhidi ya Kaizer Chiefs Mei 14.