Polisi wa Israel na Wapalestina wapambana tena

 


Polisi wa Israel wamekabiliana na waandamanaji wa kipalestina katika eneo takatifu la Jerusalem ambalo ni kitovu cha vurugu kwa majirani hao wa Mashariki ya kati. 

Makabiliano hayo yametokea leo Jumatatu. Maafisa walifyetua gesi ya kutowa machozi na maguruneti ya kurusha kwa mkono na waandamanaji wakipalestina kwa upande wao waliwarushia mawe na vifaa vyingine maafisa hao. 

Kwa mujibu wa polisi,waandamanaji walirusha mawe kutokea ndani ya uwa wa msikiti mtakatifu wa Al-Aqsa kuelekea eneo la barabara ya njia panda. 

Kwa upande wa wapalestina wamefahamisha kwamba maguruneti yalirushwa kuelekea msikitini na watu kadhaa wamejeruhiwa. 

Awali polisi iliwazuia wayahudi kutotembelea eneo hilo hii leo ambapo Waisraeli wanaadhimisha siku ya Jerusalem,tukio linalofanyika kila mwaka ambalo linatazamwa kwa kiasi kikubwa kama uchokozi wa Israel katika mji huo unaogombaniwa.


Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi