Kansela Merkel azungumza na Rais Xi Jinping kuelekea mkutano wa kilele wa G20

 


Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na rais wa China Xi Jinping, wamezungumza kwa njia ya simu hii leo, kuelekea mkutano wa kilele wa kundi la mataifa 20 yaliyostawi zaidi kiuchumi duniani G20. 

Msemaji wa serikali ya Ujerumani amesema katika taarifa kuwa Merkel na Xi wamejadili uhusiano baina ya mataifa yao, maadalizi ya mkutano wa kilele wa wakuu wa mataifa ya G20, uhifadhi wa mazingira na janga la virusi vya corona. 

Msemaji huyo ameongeza kuwa suala la haki za binadamu na makubaliano ya uwekezaji kati ya China na Umoja wa Ulaya vilijadiliwa pia katika mazungumzo hayo ya simu.


Post a Comment

0 Comments