Oct 13, 2021

Rais Putin asema Urusi itatoa gesi zaidi ikiwa Ulaya itaomba

  Muungwana Blog 2       Oct 13, 2021

 


Rais Vladmir Putin amesema leo kuwa Urusi iko tayari kutoa gesi zaidi kwa Ulaya endapo wataomba, na kutupilia mbali madai kwamba Moscow inabana ugavi wa nishati hiyo kwa malengo ya kisiasa. 

Putin ameyasema hayo katika mkutano wa gesi unaofanyika mjini Moscow.

Bei za gesi barani Ulaya zimefikia viwango vya juu kabisaa mwezi huu, lakini ikulu ya Kremlin imekuwa ikikanusha mara kwa mara madai kuwa Urusi inazuwia ugavi ili kushinikiza uidhinishaji haraka wa mradi wa bomba la gesi la Nord Stream 2 kupita bahari ya Baltic kwenda Ujerumani. 

Rais huyo wa Urusi amezitaja kama "upumbavu mkubwa", tuhuma kwamba Moscow inatumia nishati kama silaha ya kisiasa.


logoblog

Thanks for reading Rais Putin asema Urusi itatoa gesi zaidi ikiwa Ulaya itaomba

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment