Ticker

6/recent/ticker-posts

 


Mtoto wa mwaka mmoja, wengine watatu wafariki ajali ya gari

 


Mtoto mmoja wa mwaka mmoja na nusu   na watu watatu   wamefariki dunia baada ya gari dogo ya abiria  inayofanya safari kati ya  Kilwa Masoko  na  Nangurukuru mkoani Kilwa  kugongana na uso kwa uso  na  gari  mkurugenzi  wa wilaya Kilwa.


 Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi, kamishna msaidizi  Mtatiro Kitinkwi,   amethibisha kutokea   kwa ajali hiyo  ambayo imehusisha  gari dogo la mkurungenzi wa kilwa  na gari ya aina ya probox  iliyobeba abiria  ambapo  watu wanne  wamefariki dunia wakiwamo  wanawake wawili, mwanaume mmoja na mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu. Chanzo cha ajali hiyo bado hakijathibitishwa.


" Ni kweli kwamba watu wanne wamefariki  wakiwamo  mama wawili watu wazima , mwanaume mmoja mtu mzima na mtoto mmoja wenye umri wa mwaka mmoja na nusu  " amesema kamanda Kitinkwi.

Post a Comment

0 Comments