Mwanmume mmoja na mfanyakazi walimwagiliwa maji taka kutoka kwa ndege, jopo la uchunguzi lafahamishwa nchini Uingereza.
Akizungumza katika baraza la Royal Borough ya Windsor na shurika la ndege la Maidenhead, kansela Karen Davies alisema "amegutushwa" kusikia kisa hicho.
Alielezea jinsi "yeye’’ na bustani lote "lilivyofunikwa" kwa uchafu huo.
Kisa hicho kilitokea mjini Windsor kati kati ya -Julai.
Vyoo vya ndege huhifadhi maji taka katika sehemu maalum, lakini yaliyomo kawaida hutupwa mara tu ndege inapotua.
Kansela wa Clewer Mashariki aliambia kikao hicho kuwa alifahamishwa kuhusu kisa hicho cha "kuogofya" na mkazi wa eneo bunge lake, kulingana na Huduma ya Kuripoti Demokrasia ya Mitaa.
BBC imewasiliana na Mamlaka ya Usafiri wa Angani ili kupata tamko lake.