Aliyejikata uume afariki

 


Mkazi wa Kijiji cha Itolwa wilayani Chemba mkoani Dodoma, Juma Juma (34) amefariki dunia baada ya kuukata uume wake.


Inadaiwa kuwa Juma amefikia uamuzi huo wa kuukata uume wake baada ya kupata ajali na kuteguka kiuno na kusababisha asiwe rijali.


Akizungumzia juu ya tukio hilo Mwenyekiti wa kijiji hicho, Daudi Ally amesema leo Jumatatu Novemba 22, 2021 Juma amefariki baada ya kupungukiwa maji pamoja na damu.


Marehemu ameacha mjane mmoja na watoto watatu.

Post a Comment

0 Comments