Ugunduzi wa mwili uliokuwa ukioza wa msichana wa miaka mitano nchini Nigeria Hanifa Abubakar umezua wasiwasi na hisia kali, ambapo alama ya reli #JusticeForHanifa imesambaa
Mmiliki wa shule hiyo , Abdulmalik Mohammed Tanko, amekamatwa na shule hiyo kufungwa.
Alidaiwa kumteka nyara Hanifa kaskazini mwa jimbo la kano mwezi Disembaakiwa na lengo la kutaka kupewa kikombozi cha $14,600 (£10,800).
Polisi wanasema kwamba baadaye alimuua Hanifa alipogundua kwamba amemgundua.
Kulingana na mamlaka, bwana Tanko, 34, aliongoza maafisa katika ardhi ya shule hiyo ambapo alikuwa amezika mwili wa msichana huyo katika kaburi lenye kina kifupi.
Mabaki yake baadaye yalifukuliwa kwa uchunguzi wa kimatibabu na kuzikwa katika maziko rasmi na familia yake. Tanko hajafunguliwa mashtaka .
Inadaiwa kwamba Hanifa alitekwa nyaramapema mwezi Disemba nje ya shule ya kujifunza dini aliokuwa akienda.
Washukiwa wengine wawili pia wamekamatwa, maafisa wa polisi wanasema