Kylian Mbappe, 23, anajadiliana na Paris St-Germain kuhusu mkataba mpya. Mshambuliaji huyo wa Ufaransa wa miaka 23, alitarajiwa kujiunga na Real Madrid kwa uhamisho wa bure wakati mkataba wake utakapokamilika mwisho wa msimu huu. (Telegraph - subscription required)
Erling Braut Haaland anasema kuwa Borussia Dortmund inamshinikiza kufanya uamuzi kuhusu hatma yake. Klabu kadhaa za Ulaya zimehusishwa na uhamisho wa mshambuliaji huyo wa Norway wa miaka. (Guardian)
Fiorentina wanakaribia kukubali dau la £58m la Arsenal la kumnunua mshambuliaji wa matata wa Serbia Dusan Vlahovic,21. (La Repubblica - in Italian)
Bayern Munich na Barcelona wanataka kumsajili beki wa Chelsea na Denmark Andreas Christensen, 25, wakati mkataba wake utakapokamilika mwishio wa msimu huu. (Fabrizio Romano)
Mkufunzi wa Tottenham Antonio Conte, ambaye mkataba wake wa sasa unaendelea hadi mwisho wa msimu ujao,amekataa kutoa hakikisho kuhusu hatma yake ya baaadaye na kusema kuwa anazingatia jukumu lake la sasa. (Guardian)
Kiungo wa kati wa Tottenham na Ufaransa Tanguy Ndombele,25, anafanya mazoezi mwenyewe na hatma yake ya baadaye katika klabu ya Spurs iko mashakani. (Football London)
Manchester United wamewasiliana na mkufunzi wa Inter Milan Simone Inzaghi kuhusu uwezekano wa kujiunga nao msimu huu wa joto, huku Muitaliano akikaribia kuanza masomo ya kina ya lugha ya Kiingereza. (Corriere Dello Sport - in Italian)
Southampton wameulizia kuhusu usajili mlinda mlango wa Manchester United mwenye umri wa miaka 24 Muingereza Dean Henderson mwezi huu. (Football Insider)
Arsenal wamepiga hatua katika mazungumzo yao na Juventus kuhusu usajili wa mkopo wa miezi sita wa kiungo wa kati wa miaka 25-Mbrazil Arthur Melo. (Telegraph - subscription required)
Southampton wana nia ya kubadilisha mkopo wa Armando Broja kutoka Chelsea kuwa mkataba wa kudumu, ingawa huenda wakakabiliwa na ushindani wa kumnunua mshambuliaji huyo wa Albania mwenye umri wa miaka 20. (Sky Sports)
Newcastle United na Watford wanavutiwa na winga wa Nantes Mfaransa mwenye umri wa miaka 24 Ludovic Blas. (Star)
Tottenham imewapa Wolves wachezaji wanne kama sehemu mpango wa kumpata winga wa Uhispania Adama Traore, 25. (Teamtalk)
Barcelona wako tayari kumuuza mlinzi wa Marekani Sergino Dest mwenye umri wa miaka 21 mwezi huu ili kupata fedha za kumnunua mshambuliaji mpya, huku Chelsea na Bayern Munich zikimwania. (ESPN)