Ticker

6/recent/ticker-posts

 


Mkutano wa kilele wa G7 kutangaza hatua kali zaidi dhidi ya Urusi

 


Wakuu wa mataifa yatakayoshiriki mkutano wa kilele wa kundi la G7 wanaarajiwa kutangaza hatua mpya zinazolenga kuongeza mbinyo kwa Urusi baada ya kuivamia Ukraine. 

Afisa mmoja mwandamizi wa Marekani amezungumzia hatua hiyo na kuongeza kuwa siku ya Jumamosi rais Joe Biden ataungana na wakuu wenzake kutoka Uingereza, Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italia na Japan kwenye mkutano huo utakaofanyika Bavaria nchini Ujerumani. 

Baada ya kuhudhuria mkutano huo unaoanza Jumamosi hadi Jumanne, Biden atakwenda Madrid kushiriki mkutano wa kilele wa Jumuiya ya kujihami ya NATO wiki ijayo. 

Vita vya Ukraine na Urusi vinataraji kugubika makusanyiko hayo ya kidiplomasia wakati washirika hao wakiangazia namna ya kujiepusha na athari za kiuchumi zinazosababishwa na vikwazo dhidi ya Urusi na hasa suala la kupanda kwa bei ya mafuta.


Post a Comment

0 Comments