Ticker

6/recent/ticker-posts

 


Macron awaomba wanasiasa kuumaliza mkwamo nchini Ufaransa

 


Rais Emmanuel Macron ameziomba pande za kisiasa kumaliza mkwamo wa kisiasa uliosababishwa na kushindwa kwake kupata wingi wa viti katika bunge hali inayotishia kuzuia mipango yake ya mageuzi. 

Macron kwenye hotuba hiyo alionekana kuchangamkia fursa za kusonga mbele lakini hakuzungumzia suluhu yoyote madhubuti ya kufikia hapo. 

Ingawa alikiri kwamba muungano unaotawala hauna udhibiti wa kutosha na unatakiwa kujiimarisha lakini alifutilia mbali uwezekano wa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa kwa sasa. 

Kwa siku mbili zilizopita Macron alifanya mazungumzo ya nadra katika Ikulu ya Elysee, na viongozi wa upinzani akiwemo mkuu wa chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha National Rally, Marine Le Pen kutafuta njia za kutoka kwenye mkwamo huo. 

Hata hivyo kiongozi wa chama cha mrengo wa kulia cha LR Christian Jacob aliondoa uwezekano wa makubaliano yoyote na muungano wa Macron.


Post a Comment

0 Comments