Shambulizi la Urusi Kusini mwa Ukraine lamuuwa mmiliki wa kampuni ya kusafirisha nafaka


Mashambulizi makali ya Urusi yamelenga eneo la Kusini la mji wa bandari wa Mykolaiv nchini Ukraine usiku kucha na mapema leo na yamemuuwa mmiliki wa moja ya kampuni kubwa zaidi za kuzalisha na kuuza nje nafaka nchini humo. 


Haya ni kwa mujibu wa gavana wa eneo hilo Vitaliy Kim. Katika ujumbe kupitia mtandao wa telegram, Kim amesema Oleksiy Vadatursky, mwanzilishi wa kampuni ya kilimo ya Nibulon na mkewe waliuawa nyumbani kwao. 


Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amekitaja kifo cha Vadatursky kuwa hasara kubwa kwa Ukraine nzima na kusema katika taarifa kwamba mfanyabiashara huyo alikuwa katika harakati za kujenga soko la kisasa la nafaka linalohusisha mtandao wa vituo vya usafarishaji.


Wakati huo huo, Uturuki inatarajia usafirishaji wa nafaka kutoka Ukraine kuanza kesho Jumatatu. Msemaji wa Rais Recep Tayyip Erdogan amesema kuna matumaini kwamba makubaliano yaliyopatikana kwa njia ngumu yanaweza kusaidia kuzuia kuzuka kwa baa la njaa.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi