Ticker

6/recent/ticker-posts

Macron awakutanisha Kagame na Tshisekedi kujadili ukosefu wa usalama


Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amewakutanisha marais Félix Tshisekedi wa DR Congo na Paul Kagame wa Rwanda kujadili ukosefu wa usalama mashariki mwa DR Congo pembezoni mwa mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa mjini New York.


Siku ya Jumanne, Bw Tshisekedi aliikashifu vikali Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa M23 mbele ya mkutano wa Umoja wa Mataifa.


Siku ya Jumatano, Bw Kagame aliambia bunge kwamba ‘’mchezo wa kurushiana lawama hausuluhishi matatizo’’, saa chache kabla ya wote wawili kukutana chini ya mpango wa Bw Macron.


Kwa mkutano huo, Bw Kagame aliunga mkono mchakato wa kikanda kama suluhu la mzozo huo lakini akasema ‘’utahitaji usaidizi thabiti wa kifedha kutoka kwa jumuiya ya kimataifa’’.


Mamlaka za kikanda zimekubali kuunda kikosi cha kikanda ili kupambana na makundi ya waasi mashariki mwa DR Congo, bado haijafahamika ni lini kikosi hicho kitaanza hatua.


Kundi la waasi la M23 linadhibiti sehemu za Jimbo la Kaskazini mwa Congo tangu Juni.

Post a Comment

0 Comments