Maadhimisho ya siku ya UKIMWI kufanyika Lindi, TACAID yaeleza sababu.


Na Ahmad Mmow, Lindi. 

Maadhimisho ya  siku ya UKIMWI duniani ya mwaka huu kitaifa yatafanyika mjini Lindi mkoani Lindi. 


Leo akizungumza na wanahabari wa vyombo mbalimbali mjini Lindi, mkuu wa wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga alisema maadhimisho hayo kitaifa yatafanyika katika manispaa ya Lindi. Ambapo siku ya kilele mgeni rasimi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan. 


Ndemanga ambae alimuwakilisha mkuu wa mkoa wa Lindi katika mkutano huo na wanahabari alisema kabla ya siku ya ya kilele (tarehe 01.12.2022) kutakuwa na shughuli zitakazo fanyika kuanzia tarehe 24.11.2022 ambayo itakuwa siku ya ufunguzi. 


Mkuu huyo wa wilaya ya Lindi alizitaja shughuli hizo kuwa nipamoja na midahalo na mikutano ambayo itafanyika katika wiki hiyo ya maadhimisho. 


Kwaupande wake mkurugenzi mtendaji wa tume ya kudhibiti UKIMWI nchini (TACAIDS), Dkt Leornad Maboko alisema miongoni mwasababu zilizochangia maadhimisho hayo kufanyika Lindi kuwa nipamoja na mkoa huu kuwa na idadi ndogo ya maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI (VVU) na fursa za kiuchumi zilizoanza kujitokeza mkoani humu ambazo zitavutia wageni, wahamiaji na wawekezaji. 


Dkt Maboko alisema mkoa wa Lindi ni miongoni mwa mikoa michache yenye maambukizi madogo. Kwahiyo nibusara kupambana kuhakikisha maambukizi hayaongezeki. 


Alisema licha ya maambukizi madogo lakini fursa ambazo zimeanza kujitokeza zinaweza kusababisha maambukizi mapya. Kwani wageni, wahamiaji na wawekezaji wataingia na kuishi ili kutumia fursa hizo. Ikiwamo fursa zitakazotokana na ujenzi wa mtambo wa kuchakata gesi asilia ambao ni mradi mkubwa ambao thamani yake ni takribani shilingi trilioni kumi na saba. Kwahiyo kutakuwa na watu ambao baadhi yao wanaweza kusababisha maambukizi mapya. 


 Kwakuzingatia ukweli huo, Dkt Maboko alisema katika wiki ya maadhimisho hayo miongoni mwa shughuli zitakazofanyika nipamoja na midahalo na mikutano itakayo tumika kutoa elimu. Kwahiyo alitoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Lindi na jirani ya mkoa wa Lindi washiriki kikamilifu maadhimisho hayo. 


 Kuhusu hali ya UKIMWI na maambukizo nchini alisema hali ya maambukizi siyo mbaya nayanapungua. Huku akiweka wazi kwamba hadi sasa watu 1,700,000 wanaishi na Virusi Vya UKIMWI. Ambapo watu 1,500,000 kati ya hao 1,700,000 wanatumia dawa za kufubaza makali ya ugonjwa huo(ARV). 


 " Sasa tunapambana  kuzuia maambukizi mapya na kuwatafuta hao ambao wanaishi na VVU ambao hawatumii dawa ambao ni 200,000. 


 Alibainisha kwamba awali kabla ya mwaka 2021 kiwango cha maambukizi kwa mwaka kilikuwa watu 110,000. Hata hivyo mwaka 2021 kiwango hicho kilishuka na kufikia watu 54,000 sawa na asilimia hamsini. 


Alisema kundi kubwa la waathirika wa maambukizo ni vijana wa kuanzia miaka 15 hadi 24. Kwani ndio wanapata maambukizi mapya ikiwa ni asilimia 30 ya vijana wote. Huku akiwataja vijana wakike ni asilimia 80 ya vijana wanaopata maambukizi wanaopata maambukizi mapya. 


Kwakuzingatia hali hiyo mtalaam mtendaji huyo wa TACAIDS alisema zinahitajika jitihada kubwa ili kundi hilo lisiendelee kupata maambukizi mapya. 





Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi