Ticker

6/recent/ticker-posts

Marekani: Mwanamume awaua watu10' katika duka la Walmart Virginia


Mtu aliyekuwa na silaha amewaua hadi watu 10 katika duka la Walmart katika jimbo la Virginia nchini Marekani, polisi wamesema.


Ripoti zinasema kuwa mwanamume huyo ambaye ni meneja wa duka alifyatua risasi kisha akajielekezea bunduki na kujitoa uhai.


Maelezo kuhusiana na tukio hilo ni machache, lakini afisa wa polisi anasema waliouawa ni "chini ya watu 10" huku wengi kujeruhiwa.


Seneta wa jimbo la Virginia Louise Lucas alisema "amehuzunishwa sana" na kile alichokitaja kama "ufyatuaji risasi wa hivi punde zaidi wa Marekani".


Aliongeza kwenye Twitter: "Sitapumzika hadi tupate suluhu la kumaliza janga hili la utumiaji bunduki kihilela katika nchi yetu".Post a Comment

0 Comments