Mwenyekiti wa Chama cha Mapindunizi CCm Mkoa wa Tanga na Mjumbe wa kamati kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Rajab Abdalrahaman Abdalh amesema wao kama viongozi wanapona changamoto sio watu kulalamika bali ni watu wenye kushirikiana na jamii na kuzitatua changamoto hiyo.
Hayo aliyasema wakati halfa ya kuwakabidhi Timu ya mpira wa miguu ya Club ya African Sports wanakimanumanu Basi Aina ya Tata lenye thamani ua sh.milioni 170 katika timu kwa lengo kuwaunga mkono timu hiyo iweze kuondokana changamoto ya usafiri iliyokuwepo hapo mwanzo.
Aidha alisema kuwa moja ya jukumu kubwa ya chama ni pamoja kusimamia nankuendeleza michezo hususan timu za mpira wa miguu ili michezo iweze kuleta tija kwa maslahi ya jamii na taifa kwa ujumla kwani Timu ya African Sport ni timu kongwe na ya kwanza kuanzishwa katika mkoa wa Tanga tangu mwaka 1938 na ilikuwa inafanya vizuri kipindi hicho.
Alisema kutokana na changamoto mbalimbali timu hiyo iliweza kushuka na kupitwa na watani wao ambao ni mdogo wao kimchezo Coastal unioni jambo ambalo linawavunja moyo wachezaji ambapo changamoto kubwa usafiri kwa ajili ya kuwasafirisha wavhezaji na Benchi la ufundi.
"tutahakikisha timu hiyo inakuwa na uwanja wa kisasa , watajenga jengo laghorofa tatu ambalo ni jengo la timu hiyo". Alisema ustad Rajab
sambamba na hayo mwenyekiti wa CCM Mkoa waTanga aliweza kuwa kabidhi Afrian Sport kiasi cha sh.milioni 30 ambapo milioni 10 ni kwa ajilj ya bima na milioni 20 kwa ajili ya mafuta ya basi na milioni thelathini kwa Coastal unioni ili kutatua changamoto wanazozipitia.
kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Tanga Dkt Batilda Buriani amempongeza mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga kwa namna mabavyo ananihusisha na kero ya wananchi wa mkoa wa Tanga na kuzitafutia ufumbuzi jambo ambalo linazidi kufanya wananchi kuiamini serikali viongozi wake.
Kwa upande wake Rais wa TFF nchini Wales Karia alisema kuwa wao kama Chama cha mpira wa miguu Tanzania wako kuinua timu za mpira wa miguu na kuunga mkono ili ziweze kupanda daraja kwa kuimarisha viwanja vya vya michezo lakini pia ameagiza African Sports kutafutiwa kiwanja Chao kwa ajili ya kufanyia mazoezi.
Naye Naibu waziri wa michezo Hamisi Mwinjuma( MwanafA) amempongeza mwenyekiti wa CCM Mkoa waTanga kwa namba ambavyo ametoa mchango wake kwa Clabu za mpira wa miguu Mkoa wa Tanga hususan Clubu ya Coastal Union wagosi wa kaya na Africa Sports wanakimanumanu kwani ni hatua ambayo imeleta hamasa hasa kwa wadau wa michezo nchini.

0 Maoni