Makamu wa Rais Dk. Emmanuel Nchimbi ajiuzulu


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Emmanuel Nchimbi, ametangaza uamuzi wa kustaafu siasa na utumishi wa umma.

Nchimbi amesema leo, Agosti 25, 2026, amemuandikia barua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kumjulisha kuhusu uamuzi huo pamoja na nia yake ya kujiuzulu nafasi ya Makamu wa Rais.

Amesema kujiuzulu kwake kutaanza rasmi tarehe 4 Septemba 2026, akieleza kuwa amefanya uamuzi huo kwa kuzingatia matakwa ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Nchimbi ameeleza kuwa tarehe 27 Agosti 2025 alimuahidi Rais Samia kuwa angemsaidia yeye na taifa kwa uwezo wake wote na kwa uaminifu, huku akiahidi pia kuachia nafasi hiyo endapo Rais angeona anahitaji Makamu mwingine wa Rais.

“Nimejiridhisha pasipo shaka kuwa Mhe. Rais anatamani mabadiliko, hivyo nimeamua kutimiza ahadi yangu”, amesema Nchimbi.
Aidha, amemshukuru Rais Samia pamoja na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa imani waliyoonyesha kwake, huku akiwashukuru Watanzania kwa ushirikiano waliompa wakati wote aliokuwa katika utumishi wa umma.

Nchimbi amesisitiza kuwa pamoja na kustaafu siasa na utumishi wa umma, ataendelea kuwa raia mwema wa Tanzania


 

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi