Waziri wa mambo ya nje wa Iran Abbas Araghchi awasili Marekani kwenye mkutano wa UN


Waziri wa mambo ya nje wa Iran Abbas Araghchi, akiongoza ujumbe wa Tehran katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa unaoanza hii leo Jumanne hadi tarehe 28 mwezi huu. 

Araghchi ni afisa wa ngazi ya juu zaidi wa Iran kusafiri Kwenda Marekani tangu kuzuka kwa mzozo wa mashariki ya kati ambap Marekani na Israeli ziliishambulia Iran mwezi Februari.

Araghchi alizungumza kwa njia ya simu na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres baada ya kuwasili jijini Washington ambapo walijadiliana kuhusu masuala kadhaa kuelekea mkutano huo.

Awali, vyombo vya Habari vya Iran vilikuwa vimeripoti kuwa ujumbe wa Iran ungeoongozwa na Rais Masoud Pezeshkian.

Licha ya thibitisho hilo, vyombo hivyo vya Habari vilidai kuwa Marekani ilikataa kutoa visa kwa maofisa wa ujumbe ikiwemo timu yake ya mawasiliano.

Waziri huyo wa mambo ya nje wa Iran anatarajiwa pia kuwa na mazungumzo na maofisa wengine wanaohudhuria mkutano huo wakiwemo mwaziri wenzake wa mambo ya nje wa mataifa tofauti.

Licha ya kwamba Marekani imeruhusu ujumbe Iran kuingia Marekani na kuhudhuria vikao vya UN, imeweka baadhi ya marsharti kwa wajumbe hao.

Ujumbe wa Iran kwa mfano hautaruhusiwa kununua vitu vya thamani wakati ukiwa jijini New York kwa mujibu wa mamlaka nchini Marekani.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi