Haji Manara aposti hivi Instagram baada ya Yanga kupangwa na waarabu

 Baada ya ratiba ya Caf Confederation Cup kuwekwa wazi na Yanga kutakiwa kucheza dhidi ya MC Alger ya Algeria, afisa habari wa klabu ya Simba Haji Manara ame-post ujumbe kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwatania Yanga kwamba mwisho wao kwenye michuano hiyo umefika.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Manara ameandika: “Msiempenda kaja!! Kama nawaona vile Gongowazi (jina analotumia Manara siku za hivi karibuni kuwaita Yanga), safari imeshaiva hiyo na mwakani hammo.”

Yanga itaanzia nyumbani dhii ya MC Alger kati ya Aprili 7 hadi 9 kwenye uwanja taifa kabla ya kurudiana Aprili 13 hadi 15 nchini Algeria.
Mpya zaidi Nzee zaidi