Ngasa auona ubingwa Yanga

MSHAMBULIAJI wa Yanga Mrisho Ngasa, amesema ana uhakika klabu yake ina uwezo wa kurejesha ubingwa wao kutoka kwa watani zao, Simba.

Ngasa juzi aling’ara kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Malindi ya Zanzibar ambapo aliifungia bao moja na kutengeneza lingine kwenye ushindi wa mabao 2-0.

Ngasa, aliiambia Nipashe jana kuwa kama wataendeleza kasi yao waliyoanza nayo msimu huu wana nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa.

“Ligi bado mbichi, lakini kwa kasi na namna tutakavyoendelea kupambana uwanjani, nafasi ya kuchukua ubingwa ipo,” alisema Ngasa.

Ngasa, alisema wanajitahidi kufuata maelekezo ya makocha wao ambao wamekuwa na mbinu nyingi uwanjani.

“Tuna makocha wenye mbnu nyingi, kila mchezo tunakuwa na mikakati yake, hii itatusaidia kuendelea kufanya vizuri msimu huu na mwisho kuchukua ubingwa,” alisema.
Mpya zaidi Nzee zaidi