Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema kuwa anasubiri matokeo ya uchunguzi kuhusu kutoweka kwa mwandishi habari wa Saudi Arabia Jamal Khashoggi, ambaye chanzo cha habari serikalini kilisema aliuawa ndani ya ubalozi mdogo wa Saudi Arabia ulioko Istanbul.
Jamal Khashoggi mwenye umri wa miaka 59 na ambaye ni mwandishi wa habari wa gezeti la Washington Post, alitoweka baada ya miadi na maafisa wa Saudi Arabia siku ya Jumanne.
Khashoggi alienda katika ubalozi huo kutafuta vyeti vinavyohitajika kumwezesha kumuoa mchumba wake.
Chanzo cha habari kutoka serikali ya Uturuki kililiambia shirika la habari la AFP kuwa polisi wanaamini Khashoggi aliuawa ndani ya ubalozi wa Saudi Arabia mjini Istanbul, madai ambayo Saudi Arabia imeyakanusha vikali.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema atasubiri matokeo ya uchunguzi kabla kufanya maamuzi.
