Tanzania yapata uteuzi mwingine, sasa kuwa mnunuzi mkuu


Serikali ya Tanzania imeteuliwa kuwa mnunuzi mkuu wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kwa nchi 16 za jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ambapo manunuzi hayo yanaanza 9 Oktoba 2018 kupitia mkataba wa makubaliano kati ya MSD na Sekretarieti ya SADC.

Makubaliano ya ununuzi wa dawa yametiwa saini na Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya SADC Dkt.Stergomena Tax na Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya dawa MSD, Laurean Rugambwa Bwanakunu kwenye ofisi za MSD Keko Dar es Salaam.

Miongoni mwa majukumu itakayokuwa nayo Tanzania ni pamoja na kusimamia kanzidata ya dawa za nchi wanachama, kusimamia bei elekezi, kutengeneza na kusimamia mfumo wa manunuzi kwa njia ya mtandao, kutoa huduma za kitaalam na pia kutoa ushauri wa kitaalam wa masuala ya dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara.
Mpya zaidi Nzee zaidi