Rais Dkt John Pombe Magufuli amempongeza Rais Yoweri Museveni wa Uganda pamoja na wananchi wake kwa kuadhimidha miaka 56 ya Uhuru wa Taifa hilo.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter Rais Magufuli amemtumia salamu hizo za pongezi na kumuahidi Rais Museveni wa Uganda kwamba ataendelea kuukuza uhusiano na ushirikiano wa kihistoria uliopo baina ya nchi hizo mbili.
Katika ujumbe huo ambao Rais Magufuli ameutuma kwenye ukurasa wake wa Twitter amesisitiza kudumishwa kwa udugu, ujirani mwema na urafiki kwa manufaa ya Tanzania na Uganda.
