Timu zote zisizosajaliwa kufutwa


Serikali imesema klabu na vyama vyote vya michezo nchini ambavyo mpaka mwakani havitakuwa vimesajiiwa havitatambulika na badala yake zitakuwa magenge ya wahuni.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, wakati wa tamasha la michezo maalum kwa ajili ya kuathimisha Kumbukumbu ya miaka 19 tangu kufariki dunia kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Alex Nkenyenge, alisema vyama vyote pamoja klabu za michezo ni lazima visajiliwe kabla ya mwakani.

“Katika hili BMT haitafumba macho hata kidogo, lazima kila klabu ya michezo isajiliwe rasmi na kama mpaka mwakani hazitafanya hivyo hatutazitambua kwani tutawaona kama genge la watu wahuni,” alisema.

Katika tamasha hilo michezo malimbali ilifanyika ikiwamo mbio za pole maarufu kama 'jogging', soka, kukimbiza kuku na kuvuta kamba.

Nkenyenge alisema kwamba baraza lake linatekelza agizo la Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, ambaye aliagiza vyama vyote kufuata masharti hayo ikiwamo kuwa na ofisi za kudumu kwa lengo la kuzifanya ziwe na uhalali wa kufanya shughuli zao.

Mpya zaidi Nzee zaidi