Kocha wa Yanga SC ajinasibu kubeba mataji mawili msimu huu


Kocha Mkuu wa Yanga SC,  Mwinyi Zahera amesema kwa sasa anapigia hesabu za kubeba makombe yote mawili ambayo anashiriki kwa kuwa uwezo anao na nafasi ipo na wachezaji wanaonyesha nia hiyo. 

Yanga kwa sasa wanashiriki michuano ya FA pamoja na Ligi Kuu Bara ambako kote wana nafasi ya kutwaa ubingwa endapo hesabu zao zitakubali.

"Kwa sasa sioni cha kunizuia kupata matokeo, licha ya ugumu ambao ninapitia wachezaji wangu wanacheza kwa juhudi na wanajua kwamba mashabiki wanahitaji matokeo.

"Ili niweze kuwapa shukrani mashabiki nawaambia wapambane wacheze kwa nguvu kupata matokeo, hilo lipo mikononi mwao na wanafanya kitu ambacho kinaonekana hivyo bado tuna safari ya kubeba makombe yote, FA na hili la Ligi Kuu Bara," amesema Zahera.

Yanga SC ambao ni mabingwa wakihistoria Nchini  inaongoza ligi Kuu kwenye msimamo ikiwa na pointi 64 baada ya kucheza michezo 26 na kushinda mechi 20, kutoka sare mechi 4, na kufungwa mechi 2, huku ikiwa mbele ya mechi 6 dhidi ya mahasimu wao wa jadi Simba SC.
Mpya zaidi Nzee zaidi