Picha: Wanafunzi wapigwa radi wakiwa darasani, mmoja afariki


Mwanafunzi wa kidato cha Tatu katika shule ya sekondari ya Mikindani Mkoani Mtwara, Abdul Masamba, amepoteza maisha baada ya kupigwa na Radi akiwa darasani Jana huku wengine 24 wakijeruhiwa (Picha kitandani za majeruhi).

Tukio hilo limetokea majira ya saa tatu asubuhi ambalo limewakumba wanafunzi wa kidato cha tatu A wakati wakiendelea na masomo yao ambapo wanafunzi waliojeruhiwa na kupelekwa hospitali wanaeleza tukio lilivyokuwa.

Mkuu wa wilaya Mtwara Evod Mmanda anasema kuwa jumla ya wanafunzi 24 wamejeruhiwa na mmoja aliyetambulika kwa jina la Abdul Masamba amefariki dunia katika tukio hilo huku mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya Ligula Dr.Lobikieki Kissambu akisema majeruhi wote waliopelekwa hospitalini hapo wanaendelea vizuri.

Mpya zaidi Nzee zaidi