Leo Jumatano Machi 6, 2019 katika Mahakama Kuu, Bukoba itasomwa hukumu ya walimu wawili
Respicius Mtazangira na Heriet Gerald walioshtakiwa kwa kumuua mwanafunzi wa shule ya msingi Kibeta.
Walimu hao walishitakiwa kwa kumuua kwa kukusudia Sperius Eradius aliyekuwa mwanafunzi wa darasa la tano katika shule hiyo mwishoni mwa mwaka 2018.
Upande wa Jamhuri uliwasilisha mashahidi tisa katika kesi hiyo iliyosikilizwa kwa mwezi mmoja na Jaji Lameck Mlacha, ilianza Februari 6, 2019.
Inadaiwa walimu hao walitenda kosa la kumuadhibu kwa kipigo mwanafunzi Sperius Eradius kwa madai kuwa aliiba mkoba wa mwalimu Eliet kupoteza ukiwa na fedha.
