Simba amshambulia aliyemfuga


Mwanaume mwenye umri wa miaka 33 Michal Prasek ameshambuliwa na simba aliyemfuga nyumbani kwake mashariki mwa Jamhuri ya Czech

Mwanaume huyo alikuwa akimiliki Simba wawili na Simba jike alimfuga kwa sababu ya kuzalisha ambapo hatua hiyo inadaiwa kuwa ilizusha wasiwasi kwa wakazi wa eneo hilo.

Baba wa mwanaume huyo aliupata mwili wa mwanawe ndani ya kizuizi cha simba huyo na kuambia vyombo vya habari kwamba kilikuwa kumefungwa kwa ndani.

Wanyama hao waliokuwa wanaishi katika vizuizi tofuati, walipigwa risasi na kuuawa na polisi walioitwa katika eneo hilo.

Msemaji wa polisi amewaambia waandishi habari kwamba ilikuwa muhimu kwa simba hao kuuliwa ili kumfikia marehemu.

Prasek, mwenye umri wa miaka 33, alimnunua simba huyo mnamo 2016 na simba jike huyo mwaka jana, na aliwaweka wote katika vizuizi alivyovitengeneza katika ua lake katika kijiji cha Zdechov.
Mpya zaidi Nzee zaidi