Ujerumani yaigomea Urusi kurejea kundi G8

Serikali ya Ujerumani inapinga wazo la Urusi kurejea katika kundi la nchi nane tajiri duniani - G8, baada ya viongozi wa Ufaransa na Marekani kudokeza kuwa ni vyema kuiruhusu Urusi kurejea.

Msemaji wa serikali Steffen Seibert amesema kundi la G7 liliamua mwaka wa 2014 kuwa Urusi itaondolewa katika kundi hilo kufuatia hatua yake ya kuinyakua rasi ya Crimea na kuwaunga mkono wanaharakati wanaotaka kujitenga mashariki mwa Ukraine - hali ambayo inaendelea mpaka sasa.

 Seibert ameongeza kuwa kama Moscow imetoa ishara yoyote kuwa iko tayari kubadilisha msimamo wake kuhusu mzozo wa Ukraine, basi viongozi huenda wakajadili kurejea kwa Urusi.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ataandaa mkutano huo wa kilele wa G7 mwishoni mwa wiki hii, baada ya kukutana na Rais wa Urusi Vladmir Putin, akitaraji kudumisha sifa yake ya kuwa mpatanishi wa kimataifa katika wakati ambapo kuna hali ya ukosefu wa usalama wa kisiasa na kiuchumi duniani.
Mpya zaidi Nzee zaidi