Loading...

8/22/2019

WCB wavunja ukimya kuhusu Harmonize kuondoka


Meneje wa Diamond Platnumz, Sallam Sk amesema kuwa kwasasa hivi ndani ya moyo wa Msanii Harmonize haupo tena WCB baada ya kuandika barua ya kuvunja mkataba wake.

Sallam amesema kuwa kimakaratasi Harmonize bado ni msanii wa lebo hiyo, lakini kitu walichopendezewa nacho kutoka kwa msanii huyo ni kwamba amefuata sheria.

"Harmonize kwasasa hivi ndani ya moyo wake haupo WCB , Harmonize kimakaratasi bado ni msanii wa WCB ametuma barua ya kuvunja makataba wake na yuko tayari kupitia vifungu vyote vya sheria," alisema Sallam.

"Kwahiyo hicho ndio kitu ambacho tumependezewa nacho ambacho yeye mwenyewe ameridhia na ameomba kikao na uongozi tumependezewa nacho kwasababu mtu ambaye amesimama na anafuata sheria."
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger