Siku hizi mchezaji yoyote ana thamani ya euro milioni 100 bila uthibitisho wowote - Ronaldo


Mchezaji Cristiano Ronaldo anaamini katika umri wa miaka 25, angekuwa na thamani ya euro milioni 300 kwa soko la usajili la sasa.

Nyota huyo wa Juventus alijiunga na timu hiyo kwa ada ya euro milioni 112 kutoka Real Madrid majira ya kiangazi mwaka jana.

Ronado amesema kuwa soka la mpira la sasa limekuwa ni tofauti, na wachezaji wamekuwa na thamani kubwa bila ya uthibitisho wowote.

“Nitaliweka suala la Joao Felix pembeni. Siku hizi mchezaji yoyote ana thamani ya euro milioni 100 bila hata ya uthibitisho wowote. Kuna hela nyingi katika soka.

“Beki wa kati na makipa wana thamani ya euro milioni 70, euro milioni 80.
Sikubaliani na hilo, lakini hii ndio dunia tunaishi.Soko ndio lipo hivi, inabidi tuheshimu”. Ronaldo aliiambia Televisheni ya Ureno TV1

Alipoulizwa ni thamani gani angekuwa nayo akiwa na miaka 25 kwa soko la sasa, Mreno huyo alijibu “ Ni vigumu kufanya mahesabu. Kama kipa ana thamani ya euro milioni 75, mchezaji aliyefanya vile nimefanya lazima atakuwa na thamani mara tatu mpaka nne zaidi”