Naibu Waziri wa Madini 'aipa baraka' kampuni ya uchimbaji madini ya Graphite


Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo ametoa baraka kwa kampuni ya uchimbaji madini aina ya Graphite inayofahamika kwa jina la Lindi Jumbo inayofanyia shughuli zake Mkoani Lindi, kuanza ujenzi wa mtambo (Plant) na shughuli zingine zinazohitajika ili kazi ya uzalishaji ianze.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya Mkurugenzi wa kampuni hiyo bwana Allan Mulligan,  kumtembelea Naibu Waziri ofisini kwake jijini Dodoma kwa lengo la kumpa taarifa kuhusu hatua iliyofikiwa katika  mchakato wa Ujenzi wa mtambo, mabwawa ya maji taka na miundo mbinu mingine ya uzalishaji.

Mh. Nyongo ameridhishwa na taarifa hiyo iliyomfikia na kuamua kuiruhusu kampuni hiyo iendelee na ujenzi wa mtambo huo (Plant)
Mpya zaidi Nzee zaidi