Halmashauri ya mji wa Kahama yapitisha bajeti ya bilioni zaidi ya 40



Na Paschal Malulu-Kahama

Halmashauri ya mji wa Kahama mkoani Shinyanga imepitisha bajeti ya mwaka wa fedha 2020/21 kiasi cha shilingi bilioni 40,900,324,703 ikiwemo malipo ya mishara ya watumishi ndani ya halmashauri.

Katika bajeti hiyo ya fedha imejikita kuwa ya uwazi na uwajibikaji kwa watumishi pamoja na wananchi ili kuinua maendeleo ndani ya halmashauri ya mji huo ambapo fedha hiyo zaidi ya bilioni 40 mapato ya ndani pekee ni bilioni 6,579,322,750.

Akifafanua bajeti hiyo kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Kahama Clemence Mkusya amesema mishahara ya watumishi ina jumla ya shilingi bilioni 27,144,006,000, matumizi ya kawaida bilioni 1,014,598,000, elimu bila malipo bilioni 1,485,663,000 na miradi ya maendeleo ni bilioni 4,676,734,953.

Wakichangia bajeti hiyo ya mwaka wa fedha madiwani wa baraza hilo akiwemo diwani wa Kata ya Nyahanga Michael Magile kupitia chama cha mapinduzi (CCM) amesema sasa ni wajibu wa mkurugenzi kuhakikisha anasimamia mikakati ya bajeti hiyo ili fedha hiyo iweze kutumika kama ambavyo imetarajiwa ndani ya halmashauri.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha amewataka madiwani wa halmashauri hiyo kushirikiana na halmashauri kuanza mchakato wa ujenzi wa vyumba vya madarasa mapema kwani kuna dalili kufikia mwaka 2023 halmashauri ikakumbwa na uhaba wa madarasa kutokana na wanafunzi wa darasa la nne mwaka huu kuwa 14,000 walioandikishwa kufanya mtihani wa taifa hivyo mwaka 2022 watahitihimu darasa la saba.

Amesema serikali ya awamu ya tano imeonesha matunda ya watoto kusoma kwa wingi kwa muda huu iliyokaa madarakani kwani kila mwaka wanafunzi wanaongezeka hivyo mwaka 2023 wanafunzi 14,000 wakihitimu watakaofaulu watakuwa asilimia kubwa ambayo inaweza kusababisha kukosa madarasa hivyo madiwani wakianza kampeni mapema kwa kushirikiana na wananchi pamoja na wananchi kuanza kujenga madarasa itasaidia kwani kufikia mwaka huo madarasa yatakuwepo yakutosha.
Mpya zaidi Nzee zaidi