Umoja wa Mataifa waonya juu ya silaha za nyuklia

Mwakilishi mkuu wa Umoja wa Mataifa katika kuondokana na silaha, Izumi Nakamitsu amesema kwamba ile hali ya kujimilikisha silaha za kinyuklia bila mipaka imerudi tena.

Katika taarifa ya maandishi iliyotolewa na Umoja wa Mataifa, Nakamitsu akihutubia baraza la uslama la Umoja wa Mataifa alisema kupitia mkutano huo wanaweza kuanza kufikiria ni jinsi gani wanaweza kukabiliana na hatari za silaha za kinyuklia.

Nakamitsu akikumbushia kuhusu mkataba wa mwaka 1970 wa kuzuia kuenea kwa silaha za kinyuklia (NPT) alisema kwamba huo ndio ulikuwa mkataba pekee unaoyataka mataifa yenye silaha za kinyuklia kwenye maghala yao kuondokana na silaha hizo.

 Izumi Nakamitsu katika mazungumzo yake alisema,

"Katika siku za hivi karibuni hotuba za kusifu silaha za nyuklia zimekuwa zikiongezeka hii inaongeza hatari na kupunguza utulivu. Tunapaswa kurudi katika mawazo ya Rais Ronald Reagan ( wa Marekani) na Rais Mihail Gorbachov (wa Urusi). Hakuna aayeweza kushinda katika vita vya kinyuklia. Na vita vya namna hiyo ni bora kuviepuka”.

Makubaliano ya NPT yanazuia uundaji wa silaha mpya za nyuklia sanjari na kutaka kuangamizwa kabisa kwa silaha za namna hiyo siku za usoni.
Mpya zaidi Nzee zaidi