Taarifa zilizotolewa na kituo cha kuzuia maradhi nchini Korea Kusini zimeonesha nchi hiyo imerikodi visa vipya 297 vya COVID-19 katika kipindi cha saa 24 zilizopita, idadi ambayo ni kubwa kuwahi kushuhudiwa ndani ya siku moja tangu mnamo mwezi Machi.
Hiyo ni siku ya sita mfululizo kwa nchi hiyo kurikodi maambukizi ya tarakimu tatu huku visa vingi ni kutoka katikatia ya mji wa Seoul, ambako wafanyakazi wa afya wanafanya juhudi za kupambana na kusambaa kwa virusi vya corona.
Hivi sasa maafisa wa Korea Kusini wanatekeleza hatua kali za kuwalazimisha watu kujitenga katika mji huo mkuu, jimbo jirani la Gyeonggi na mji mwingine wa Incheon na mikusanyiko ya watu 50 katika makaazi na watu 100 kwenye maeneo ya wazi imepigwa marufuku.
