Maambukizi ya virusi vya corona yanapanda nchini Ujerumani

 

Ujerumani imerikodi visa vipya 1,510 vya maambukizi ya virusi hatari vya corona ndani ya saa 24 zilizopita, idadi ambayo ni kubwa kuwahi kuripotiwa katika kipindi cha miezi mitatu iliyotangulia. 

Taarifa hizo zimetolewa leo na kituo cha udhibiti wa maradhi ya kuambukiza cha Robert Koch na kufanya idadi ya watu walioambukizwa virusi vya corona nchini Ujerumani kupindukia 226,000 pamoja na vifo vya watu 9,243. 

Idadi ya visa vya virusi vya corona nchini Ujerumani imekuwa ikipanda katika wiki za hivi karibuni na katika siku kadhaa zilizopita maambukizi ya kila siku yamepindukia visa 1,000. 

Mapema jana, Kansela Angela Merkel alitoa wito kwa wajerumani kuzingatia masharti yaliyowekwa kupambana na kusambaa virusi vya corona, akionya hakuna vizuizi vitakavyoondolewa nchini humo ikiwa idadi ya maambukizi itaendelea kupanda.


Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi