Nov 25, 2021

Fahamu mjama 638 za mauaji alizoepuka Fidel Castro

  Muungwana Blog       Nov 25, 2021

 


Fidel Castro alioongoza Cuba kama taifa lililoamini uongozi wa chama kimoja kwa takriban nusu karne kabla ya kifo chake 2016 akiwa na umri wa miaka 90.


Huku mataifa yaliokuwa yakitawaliwa kikomyunisti yakianguka , Castro aliendeleza utawala huo licha ya ukosoaji mkubwa kutoka kwa adui wake mkubwa Marekani.


Akiwa mtu aliyependwa na wengi na pia kupingwa na wengi , mashabiki wake walimpongeza kwa kuwa bingwa wa mfumo wa Kisosholisti na mtu ambaye alilirudisha taifa hilo kwa raia.


Na huku Cuba ikiwa inaadhimisha miaka mitano tangu kifo cha kiongozi huyo , BBCswahili inaangazia njama 637 za mauaji yake alizoziepuka.


Njama ya kutumia sigara kumuua Fidel Castro ambayo ilitibuka inajulikana sana, lakini njama nyengine 637 dhidi ya maisha yake ni zipi?


Shirika la kijasusi nchini Marekani CIA na watu waliotoroka Cuba wakati wa uongozi wa Castro walitumia nusu ya karne moja kufanya njama za kumuua kiongozi ambaye taifa lake lina athari kubwa kwa Marekani, kulingana na balozi wa Marekani nchini Cuba Wayne Smith.


Wasifu wa Fidel Castro

Wakati mmoja kiongozi huyo wa Cuba alinukuliwa akisema, iwapo kuepuka majaribio ya mauaji kungekuwa miongoni mwa michezo ya Olimpiki ningejishindia medali ya dhahabu.


Hatahivyo baadhi ya njama hizo hazikutekelezwa ,kulingana na aliyekuwa mlinzi wa zamani wa Fidel Castro, Fabian Escalante.


Stakhabadhi zilizofichuliwa wakati wa utawala wa Bill Clinton zilionyesha kuwa CIA wakati mmoja walianza kuwafanyia utafiti konokono wa eneo la Carebean.


Njama, ilikuwa kutafuta konokono mmoja ambaye angemvutia Castro anayependa sana kuogelea na kumjaza vilipuzi ndani yake kabla ya kumlipua Castro atakapomshika


Mpango mwengine ulikuwa ule wa kutengeza boya la kuogelea ambalo huvaliwa kama shati na ambalo lingetiwa ugonjwa mbaya wa ngozi ili kumuathiri kiongozi huyo.


Ajenti huyo alisikitika na akataka mpango mwengine ambao sio rahisi kuugundua, ripoti hiyo ilisema.


Mmoja ya wapenzi wa Castro wa zamani ,Marita Lorenz alisajiliwa.


Alipewa dawa zenye sumu ili kuweka katika kinywaji cha Castro. Lakini Castro aligundua jaribio hilo na anadaiwa kumpatia bunduki yake badala yake atumie kumuua.


''Huwezi kuniua. Hakuna anayeweza kuniua Bi Lorenzo'', Bw Castro alimwambia, alipokuwa anahojiwa na gazeti la New York daily.


Castro alidaiwa kutabasamu na kuendelea kuvuta sigara yake.''Nilijihisi nimetolewa pumzi kwa sababu alikuwa na uhakika juu yangu. Alinikumbatia na tukafanya mapenzi''.


Jaribio jingine lililokuwa maarufu dhidi ya maisha ya Castro ni lile la 2000, wakati ambapo mpango uliwekwa kuweka vilipuzi vingi katika jukwaa ambalo alitarajiwa kuhutubia nchini Panama.


Mpango huo ulitibuliwa na vikosi vya usalama vya Castro.


Watu wanne ikiwemo mtoro mmoja wa Cuba pamoja na ajenti wa CIA kwa jina Luis Posada walifungwa lakini baadaye wakaachiliwa.


Pia kulikuwa na mipango ya kumfanya Castro ambaye pia anajulikana '' The Beared'' aonekana kama chombo cha kukejeliwa badala ya kumuua.


Mpango mmoja ulikuwa kumwagia viatu vyake chumvi ya thallium wakati wa ziara yake ya ughaibuni kwa lengo kwamba anaposhika ndevu zake zingeweza kukatika.


Lakini mpango huo ulitibuliwa baada ya Castro kuahirisha ziara hiyo.Castro alichukua tahadhari ya hali ya juu ili kuwakwepa watu waliopanga mauaji yake.


Mwaka 1979 alipokuwa akielekea mjini New York ili kuhutubia mkutano wa Umoja wa Mataifa hakuweza kuwazuia wanahabari waliomuuliza iwapo alikuwa amevaa fulana ya ndani ambayo ina kinga dhidi ya risasi, alivua shati lake na kuwaonyesha kifua chake.


Miongo kadhaa awali mwaka 1975, tume ya bunge la seneti nchini Marekani ilifichua maelezo ya njama nane dhidi ya maisha ya Castro kwa kutumia vifaa ambavyo tume hiyo inasema ''vinachosha akili''.


Njama moja iliopangwa na ambayo karibu ifaulu mara mbili ilikuwa ile ya kutuma dawa za sumu Cuba na kuwapeleka watu kumuua kiongozi huyo.


Ulikuwa wakati kama huo ambapo rais Kennedy, ambaye aliruhusu uvamizi wa kumuondoa madarakani rais Castro mwaka 1961 aliuawa, ambapo ajenti wa CIA alikuwa anatoa kalamu yenye sumu ilio na sindano kwa ajenti mmoja wa Cuba ili kumuua kiongozi huyo.

logoblog

Thanks for reading Fahamu mjama 638 za mauaji alizoepuka Fidel Castro

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment