Nov 25, 2021

Waziri Simbachawene azindua alama za barabarani akitaka zitumike kwa usahihi

  Muungwana Blog       Nov 25, 2021


Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachewene amezindua alama maalumu kwenye barabara kwa waendesha pikipiki (buffer Zones) katika maeneo sita jijini Arusha, akitaka zitumike kwa usahihi ili kupunguza ajali.


Uzinduzi wa alama hizo uliodhaminiwa na  Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) unatarajiwa kusaidia kupunguza ajali za watembea kwa miguu na pikipiki.


Akizuznguindua baada ya kuzindua alama hizo, Waziri Simbachawene alisema Serikali imejitolea kuboresha usalama wa barabara kwa wote na kuhakikisha barabara zetu ni za kisasa.


“Serikali kwa ujumla na Wizara ya Mambo ya Ndani tunajivunia kushirikiana na TBL na tutaendelea kuunga mkono jitihada za kuimarisha usalama wa barabara nchini Tanzania na kuhakikisha watumiaji wote wanatumia barabara salama,” alisema.


Maeneo hayo yenye alama maalum ni pamoja na yenye idadi kubwa ya ajali za barabarani na vifo vinavyohusisha waendesha pikipiki na makutano yanayotumiwa na idadi kubwa ya waendesha pikipiki na watembea kwa miguu, yakiwemo ya Philips Junction, Sanawari Junction, Sakina Junction, Mbauda Junction, Mianzini Junction na Nairobi Road Junction.


Naye Meneja wa Tanroads, Mhandisi Christina Kayoza alisema “Tanroads inaamini uanzishaji wa maeneo ya barabara yenye alama maalum kwa waendesha Pikipiki utakuwa na mafanikio kama yaliyopatikana São Paulo nchini Brazili, ambapo kati ya 2013 na 2015 takribani kanda 350 zilianzishwa katika jijini hilo, kanda 54 kati ya hizo zikifuatiliwa na kuonyesha  kwa kasi kubwa zimefanikisha kupunguza matukio ya ajali na majeruhi wa ajali za pikipiki.”


Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TBL, Jose Moran alisema alisema watashirikiana na Tanroads ili kupata ushirikiano kati ya mawakala wa elimu na uhandisi ili kusaidia askari wa usalama barabarani kuwaelekeza watumiaji wa barabara (waendesha pikipiki, magari, baiskeli, watembea kwa miguu jinsi ya kutumia maeneo haya kwa ajili ya usalama wao.

 

"Kwa kuzingatia kwamba utumiaji wa  mfumo huu  ni mpya, tunaelewa kuwa watumiaji wa barabara hawawezi kuelewa jinsi ya kutumia maeneo haya bila maelekezo. Kwa maana hiyo, inapendekezwa kuwa utumiaji wa  maeneo haya ufanywe kwa ushirikiano sambamba na kufanya jitihada za kutoa elimu,” aliongeza Moran.

logoblog

Thanks for reading Waziri Simbachawene azindua alama za barabarani akitaka zitumike kwa usahihi

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment