Katika jitihada endelevu za kuboresha huduma za mawasiliano kwa wateja wetu nchini, Airtel Tanzania leo imezindua promosheni mpya ya ‘JiBoost na Airtel Money’ ambayo inawapa nafasi watumiaji wa Airtel Money kujipatia shilingi 20,000 taslim ya supa bonasi kupitia miamala ya kila siku watakayofanya. Mpango huu ni sehemu ya maono ya kampuni ya Airtel kupanua huduma ya Airtel Money na kujenga huduma za kifedha jumuishi na wezeshi kwa wateja wake.
Akizungumza wakati wa uzinduzi, Mkurugenzi wa Airtel Money, Andrew Rugamba alieleza furaha yake kuhusu kampeni ya JiBoost na Airtel Money akisema kuwa, “Tunafurahia kuitambulisha kampeni hii ya “JiBoost na Airtel Money’ ili kuleta thamani kwa wateja wetu.
Promosheni hii imetengenezwa kuwazawadia wateja wetu kila wanapotumia huduma za Airtel Money katika Maisha yao ya kila siku kama manunuzi ya vifurushi vya muda wa maongezi, intaneti, au malipo ya serikali kama vile LUKU. Wateja wetu watakuwa wakinufaika zaidi na kila muamala watakaofanya. Tunajivunia kuwa vinara wa kutoa huduma suluhishi kupitia Airtel Money kwa wateja wetu.”
Akielezea kampeni ya JiBoost na Airtel Money, Balozi wa Airtel Tanzania, Diamond Platnumz alieleza furaha yake kuhusu kampeni hiyo.
“Airtel Money siku zote imekuwa ikirahisisha maisha. Jiboost inakupa wepesi wa kufanya miamala pamoja na kurejeshewa fedha kwenye akaunti yako. Hii ni fursa kwetu sote ya kutunza na kupata fedha wakati tukiendelea kufanya matumizi. Najivunia kuwa sehemu ya mapinduzi haya,” alisema.
Kwa upande wake, Joti ambae alivaa uhusika wa Mr Money, alisema, “Kama Mr Money, naweza kukuambia kuwa kampeni hii ni mahususi kwa ajili ya kurudisha pesa kwenye mfuko wako. Kila utakapofanya malipo ya TV, umeme na kununua muda wa maongezi, unakuwa unajipa nafasi kubwa zaidi ya kupata bonasi. JiBoost ipo hapa kwa ajili ya kufanya miamala yako ya kila siku iwe ya furaha na yenye zawadi.”
Kampeni ya JiBoost ya Airtel Money inamruhusu Mteja kuweza kupata supa bonasi ya shilingi 20,000 kupitia muamala unaotumwa Kwenda kwa mtu mwingine, kununua muda wa maongezi, kununua vifurushi, malipo ya LUKU, malipo ya serikali na kununua vifurushi vya king’amuzi. Wateja pia wanaweza kupata bonasi hiyo kwa kufungua App ya Airtel Money.
Kila mteja atakapokamilisha muamala unaostahili, atapokea ujumbe wa maandishi ukithibitisha kuwa amepata bonasi. Kila mteja atakapokuwa akifanya malipo atakuwa anapata gawio la bonasi hadi itakapofikia thamani ya shilingi 20,000. Kila bonasi atakayopata mteja itaonekana kwenye akaunti yake ya Airtel Money ikiambatana na ujumbe wa SMS utakaoonyesha mwenendo wa bonasi hizo.
Ili kuweza kunufaika na ofa hii, wateja wa Airtel wanaweza kupiga *150*60# au kutumia App ya MyAirtel kukamilisha miamala na kuanza kujizolea bonasi kupitia kampeni ya JiBoost na Airtel Money.
0 Comments