Jeshi la Polisi Mkoa wa Rukwa limesema linafanya uchunguzi kuhusu madai ya Giles George Nandi, mkazi wa Wilaya ya Nkasi, ambaye anadaiwa kufungwa pingu kwa muda wa siku tatu bila sababu.
Jeshi hilo limesema limeanza kukusanya ushahidi ili kubaini askari anayehusishwa na tukio hilo, na endapo ukiukwaji wa sheria utabainika, hatua stahiki za kinidhamu na kisheria zitachukuliwa.
Hatua hiyo imekuja baada ya kusambaa kwa picha mjongeo katika mitandao ya kijamii, ikimuonesha Giles akiwa amefungwa pingu, ambapo Jeshi la Polisi limesisitiza kuwa hakuna aliye juu ya sheria na atakaye bainika kufanya kitendo hicho hatua stahiki za kisheria zitachukuliwa.
